Kinyangatom

Kinyangatom ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Ethiopia inayozungumzwa na Wanyangatom. Kinyangatom kinafanana sana lugha ya Kitoposa nchini Sudan Kusini na lugha ya Kiturkana nchini Kenya. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kinyangatom imehesabiwa kuwa watu 24,300. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kinyangatom iko katika kundi la Kinilotiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy